Home » Tanzania yasaini makubaliano na Boeing kuongeza ufanisi wa ndege zake

Tanzania yasaini makubaliano na Boeing kuongeza ufanisi wa ndege zake

by Joshua Kiziba

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imesaini makubaliano mapya na kampuni ya uundaji wa ndege, Boeing kwa ajili ya kutumia huduma ya Fleet Link.

Kupitia makubaliano hayo, ATCL itaweza kupokea taarifa muhimu za uendeshaji wa ndege zake, Boeing 737-9 na Boeing 787-8, kwa njia ya mtandao (wireless) mara baada ya kila safari.

Teknolojia hiyo itasaidia kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa ndege, kurahisisha kazi za kiufundi, na kupunguza gharama za usimamizi pamoja na usasishaji wa mifumo ya ndege.

ATCL ilisaini mkataba huo wakati wa mkutano wa African MRO 2026 uliyofanyika Adid Ababa nchini Ethiopia.

Mkutano huo uliofanyika kuanzia 29 hadi 31 Machi 2026 ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika barani Afrika ukiilenga moja kwa moja sekta ya matengenezo ya ndege (MRO – Maintenance, Repair and Overhaul), na uliyakutanisha mashirika ya ndege mbalimbali, wahandisi na wataalamu wa anga kujadili namna ya kuboresha huduma hizo barani Afrika.