Home ยป Tanzania yaweka mikakati kuhakikisha rasilimali zinawanufaisha wananchi wote

Tanzania yaweka mikakati kuhakikisha rasilimali zinawanufaisha wananchi wote

by Joshua Kiziba

Serikali ya Tanzania imepiga hatua nyingine katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wake kwa vitendo ambapo imefanya mazungumzo ya kimkakati na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dhahabu Duniani (WGC), David Tait.

Baadhi ya Mambo makuu yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni pamoja na;

I. Uongezaji Thamani (Value Addition): Kusisitiza sera ya kutokubali kusafirisha dhahabu ghafi nje ya nchi. Lengo ni kuvutia uwekezaji wa viwanda vya kusafisha na kutengeneza bidhaa za dhahabu hapa nchini.

II. Urasimishaji wa Wachimbaji Wadogo: Mpango wa kuwawezesha wachimbaji wadogo (ambao wanachangia 40% ya uzalishaji) kufanya kazi kwa tija na kuzingatia mazingira.

III. Ushirikiano wa Kimataifa: WGC imevutiwa na mfumo wa Tanzania na kuichagua kuipa ushirikiano wa kukuza sekta ya madini, kwa kuwajengea uwezo, maarifa na teknolojia wachimbaji wadogo ili iwe kitovu (hub) cha mfano wa namna ya kukuza sekta ya dhahabu.