Home ยป Wasichana 13,000 waliokatisha masomo warejea shule

Wasichana 13,000 waliokatisha masomo warejea shule

by Joshua Kiziba

Zaidi ya wasichana 13,000 wenye umri kati ya miaka 13 na 21 waliokatisha masomo ya sekondari kwa sababu mbalimbali wamejisajili na kurudi shuleni kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari kwa Njia Mbadala (SEQUIP-AEP) ulioanza mwaka 2022 na kufikia mwaka 2026.

Watoto hao waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mimba za utotoni, ajira za watoto, kuolewa kabla ya wakati na hali za kiuchumi za familia, sasa wanaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, vyuo vya kati na vyuo vikuu.