Tanzania ni Jamhuri ya muungano iliyoundwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964. Lakini ni taifa lenye historia ndefu. Haya ni baadhi ya matukio makuu historia ya taifa hili.
1498 – Mreno Vasco da Gama afika pwani ya Tanzania.
1506 – Wareno wafanikiwa kudhibiti maeneo karibu yote ya pwani ya Afrika Mashariki.
1699 – Wareno wafurushwa kutoka Zanzibar na Waarabu kutoka Oman.
1884 – Shirika la German Colonisation Society lililoanzishwa na Mjerumani Carl Peters laanza kuchukua umiliki wa maeneo Tanzania bara.
1886 – Uingereza na Ujerumani zatia saini mkataba wa kuruhusu Ujerumani kudhibiti maeneo ya Tanzania bara ila tu ukanda mwembamba maeneo ya pwani ambao unasalia chini ya sultani wa Zanzibar. Zanzibar yaendelea kuwa nchi lindwa ya Uingereza.
1905-06 – Wapiganaji wa Maji Maji washindwa na wanajeshi wa Ujerumani.Kutawaliwa na Uingereza
1916 – Wanajeshi wa Uingereza, Ubelgiji na Afrika Kusini washinda wanajeshi wa Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na kukalia Afrika Mashariki ya Kijerumani. (Eneo la Afrika Mashariki ya Kijerumani lilijumuisha Tanganyika na Rwanda na Burundi).
1919 – Muungano wa Mataifa waiteua Uingereza kuwa mdhamini wa Tanganyika – ambayo sasa ndiyo Tanzania bara.1929 – Chama cha Tanganyika African Association (TAA) chaanzishwa.
1946 – Umoja wa Mataifa wabadilisha idhini ya Uingereza Tanganyika kutoka kwa mdhamini hadi kuwa mlezi.
1954 – Julius Nyerere na Oscar Kambona wabadilisha chama cha Tanganyika African Association kuwa Tanganyika African National Union (TANU).
Uhuru1961 – Tanganyika yajipatia uhuru Julius Nyerere akiwa waziri mkuu.
1962 – Tanganyika yawa jamhuri Nyerere akiwa rais.
1963 – Zanzibar yajipatia uhuru wake.
1964 – Sultani wa Zanzibar apinduliwa na chama cha Afro-Shirazi Party kwenye mapinduzi ya mlengo wa kushoto yaliyokuwa na ghasia; Tanganyika na Zanzibar zaungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nyerere akiwa rais wa jamhuri hiyo mpya na kiongozi wa serikali ya Zanzibar na kiongozi wa chama cha Afro-Shirazi Party, Abeid Amani Karume, akiwa makamu wa rais.

Maandalizi ya uchimbaji wa visima vitatu vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay kilichopo Mkoani Mtwara yanaendelea vizuri ambapo hadi kufikia Februari 03, 2026, maandalizi yalikuwa yamefikia zaidi ya asilimia 90.