
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Dar es Salaam: Tanzania is demonstrating strong economic resilience despite rising global oil tensions linked to instability in the Middle East, with the government taking strategic measures to cushion citizens from severe shocks. While fuel prices have recently increased to above Sh3,800 per litre, authorities maintain that the country remains well-positioned to withstand the pressure.
The government’s proactive planning, including maintaining strategic fuel reserves and ensuring steady supply chains, has helped stabilise the situation in the short term. Officials emphasise that the price adjustments reflect global market dynamics rather than domestic shortages, underscoring Tanzania’s continued energy security.
Experts note that Tanzania’s unique energy structure provides a natural buffer. With over 85 percent of energy consumption derived from biomass and minimal reliance on oil for electricity generation, the country is less exposed to global oil disruptions compared to more industrialised economies.
In addition, Tanzania’s economy remains largely insulated due to its modest dependence on heavy manufacturing. Most industries rely minimally on fuel, while localised supply chains for food and essential goods help contain the impact of rising transport costs.
The government’s continued commitment to monetary discipline has also played a key role, with inflation remaining below 5 percent for over a decade. This stability provides confidence that current price pressures will be managed without triggering broader economic instability.
With ongoing diplomatic efforts globally expected to ease tensions, Tanzania is projected to navigate the current crisis without major disruption, reinforcing confidence in the country’s economic management and long-term resilience.
Dar es Salaam: Air Tanzania Company Limited (ATCL) has expressed strong confidence in its path to financial stability, projecting a break-even point by 2027 as ongoing reforms, rising revenues and improved operational efficiency continue to reshape the national carrier.
Speaking in an interview, ATCL Managing Director and CEO, Peter Ulanga, said the airline has entered a new phase of recovery, with clear indicators that its turnaround strategy is gaining momentum. “We are reviewing our projections, but most likely we do not expect to go beyond 2027 without breaking even,” he noted.
The airline’s optimism is backed by a significant surge in revenues, which increased by over Sh143 billion between the 2023/24 and 2024/25 financial years, with further growth of more than Sh200 billion projected this year. This steady upward trajectory reflects the success of reforms implemented under the government’s strategic revival plan.
Operational efficiency has also improved markedly, particularly in flight reliability. ATCL has recorded minimal cancellations and now achieves about 90 per cent on-time departures within 30 minutes, a move that has strengthened customer confidence and service delivery.
A key driver of growth has been the airline’s expansion into international routes and cargo services. Strong demand on routes such as China and Mumbai, alongside the introduction of charter cargo operations, has boosted revenues and shifted the airline toward more profitable markets.
With continued government support, strategic investments and expanding global connectivity, ATCL is positioning itself as a competitive regional carrier and a future Pan-African aviation player, contributing significantly to Tanzania’s economic growth and international presence.
Tanzania imetajwa kuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya wakulima wadogo wa kahawa.
Hilo limebainishwa na Umoja wa Wadau wa zao la Kahawa Duniani (ICP) wakati ukitimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, ambapo umeangazia mafanikio katika kuboresha maisha ya wakulima hao wadogo wa kahawa duniani.
Kwa mujibu wa Morgan Mkonyi, Meneja Mwenza wa Shirika la Hanns R. Neumann Stiftung (HRNS) Tanzania, mafanikio ya ICP yanaonekana moja kwa moja katika maisha ya wakulima wa kahawa nchini.
“Kwa Tanzania, miaka 25 ya ICP si tu kumbukumbu ya mafanikio, bali ni ushahidi wa mabadiliko halisi katika maisha ya wakulima wadogo. Kupitia mafunzo, ushirikiano na uwekezaji wa muda mrefu, wakulima wameongeza uzalishaji, wameimarisha ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na wameboresha maisha yao kwa ujumla,” amesema Mkonyi.
Ameongeza maadhimisho hayo pia ni fursa ya kuendeleza dhamira ya kuwawezesha vijana kuingia na kunufaika na sekta ya mnyororo wa kahawa.
Tofauti na miradi mingi ya kilimo inayolenga uzalishaji pekee, ICP imekuwa ikitekeleza mkakati wa jumla unaojumuisha nyanja mbalimbali za maisha ya mkulima.
Mbinu hiyo inahusisha maendeleo ya biashara za familia, uimarishaji wa vikundi vya wakulima, usawa wa kijinsia, ushiriki wa vijana, pamoja na mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Tangu kuanzishwa kwake, zaidi ya familia 125,700 za wakulima katika nchi 13 zinazozalisha kahawa zimefikiwa na miradi ya ICP.
Wakulima wamewezeshwa kutumia mbinu bora za kilimo, pamoja na kupanua shughuli zao kwa kulima mazao mengine ili kuongeza usalama wa chakula na kipato cha ziada.
Aidha, ICP imechangia kuanzishwa na kuimarishwa kwa zaidi ya vyama na ushirika wa wakulima 2,700, hatua iliyowawezesha kupata huduma muhimu na soko lenye ushindani.
Aidha, katika juhudi za kuhakikisha ushirikishwaji, ICP imeweka mkazo katika kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika uamuzi.
Takwimu za mwaka 2025 zinaonesha asilimia 45 ya washiriki wa mafunzo walikuwa wanawake, huku asilimia 22 wakiwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35.
Kwa mujibu wa Rui Miguel Nabeiro, Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya ICP, ushirikiano huo umefanikiwa kwa sababu ya kuunganisha maarifa, rasilimali na uzoefu kwa lengo la pamoja la kuboresha maisha ya wakulima.
Katika kipindi cha miaka 25, wanahisa sita wa ICP wamewekeza Euro milioni 25 katika shughuli za ICP, na kuvutia rasilimali za ziada kutoka mashirika ya wafadhili na washirika wengine ili kuendeleza suluhisho zenye ufanisi zinazoleta mabadiliko ya kweli na yenye tija katika sekta ya kahawa.
Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, sekta ya kahawa bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za uzalishaji, pamoja na kupungua kwa misaada ya kimataifa katika baadhi ya nchi.
Kutokana na hali hiyo, ICP imeeleza itaendelea kushikilia mkakati wake wa muda mrefu wa uwekezaji na ushirikiano, ili kuhakikisha mabadiliko endelevu katika sekta ya kahawa yanaendelea kupatikana.
Kwa ujumla, mafanikio ya ICP ndani ya miaka 25 yanaifanya Tanzania kuwa mfano hai wa namna ushirikiano wa kimataifa unavyoweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo na maisha ya jamii za wakulima.
Sekta ya afya nchini imepiga hatua kubwa kufuatia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuanza kutumia maabara ya kisasa yenye teknolojia ya roboti ya thamani ya shilingi bilioni 5.5 inayotarajiwa kuleta mapinduzi katika upimaji wa magonjwa mbalimbali hususan ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge alisema maabara hiyo ni miongoni mwa maabara kubwa na za kisasa zaidi katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa na uwezo wa kupima sampuli kwa haraka na usahihi wa hali ya juu kwa wagonjwa wa ndani na nje ya taasisi hiyo.
Alisema uwekezaji huo mkubwa wa Serikali umeongeza ufanisi wa huduma huku ukipunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya kibinadamu katika uchunguzi wa maabara.
Aliongeza kuwa teknolojia hiyo ina uwezo wa kuchakata idadi kubwa ya sampuli kwa muda mfupi, hatua inayochangia kupunguza muda wa mgonjwa kukaa hospitalini ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi zaidi.
Mbali na utoaji wa huduma, Dkt. Kisenge alisema maabara hiyo pia inatumika kama darasa hai kwa wataalamu wa afya nchini kwaajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu.
Katika hatua nyingine, Dkt.Kisenge alibainisha kuwa JKCI inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia ya akiliunde (Artificial Intelligence) ambapo mwaka 2024 walizindua mfumo wa kisasa unaowezesha kufuatilia hali ya mgonjwa akiwa nyumbani kwa kutumia kifaa maalumu cha Dozee.
Alifafanua kuwa teknolojia hiyo hutumia shuka maalumu ambalo huwekwa chini ya godoro la mgonjwa na kumwezesha daktari kufuatilia viashiria muhimu vya afya ikiwemo mapigo ya moyo, upumuaji na presha bila mgonjwa kufika hospitali.
“Tangu kuanzishwa kwa huduma hii wagonjwa zaidi ya 100 wamenufaika. Tunatarajia kupanua zaidi matumizi ya teknolojia hii ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa walioko mbali na vituo vya huduma za afya”, alisisitiza Dkt. Kisenge.
Mkurugenzi huyo alisema JKCI imeanzisha mfumo wa kisasa wa kuweka miadi kwa njia ya mtandao (online booking) ambayo ilianza kutumika mwaka 2025, ambao hadi sasa imeshahudumia wagonjwa zaidi ya 71,506. Mfumo huo unawawezesha wagonjwa kuchagua muda wa kuonana na daktari na hivyo kupunguza msongamano na muda wa kusubiri huduma.
Taasisi hiyo pia imeanzisha mfumo wa usajili wa ndugu wanaotembelea wagonjwa waliolazwa (visitors management system), unaolenga kuimarisha usalama na uratibu wa huduma wodini.
Dkt. Kisenge alieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26, JKCI inalenga kuboresha zaidi huduma za tiba mtandao (telecardiology) ili kupanua wigo wa huduma za kibingwa katika hospitali za kanda na mikoa nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maabara wa JKCI Thadei Kavishe alisema maabara hiyo ina uwezo wa kupima zaidi ya sampuli 5,000 kwa saa moja.
“Tunapima aina mbalimbali za sampuli ikiwemo damu, mkojo na majimaji kutoka sehemu mbalimbali za mwili kama moyo, mapafu na tumbo”, alisema Kavishe.
Aliwataka wadau wa sekta ya afya zikiwemo hospitali nyingine kutumia huduma za maabara hiyo kwa kuleta sampuli zao kwa uchunguzi wa uhakika na wa kisasa.
Baadhi ya wagonjwa wanaopata huduma katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wameelezea kuridhishwa na maboresho ya huduma yanayotokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa hususan maabara ya roboti na mifumo ya tiba mtandao.
“Zamani nilikuwa nasubiri majibu kwa muda mrefu, lakini sasa ndani ya saa moja tayari unapata majibu. Inasaidia sana kupunguza wasiwasi na kuanza matibabu mapema, huduma ya maabara imekuwa ya haraka na yenye uhakika zaidi kuliko ilivyokuwa awali”, alisema Mama Asha Mussa mkazi wa Dar es Salaam.
“Maabara ya kisasa imeongeza imani kwa wagonjwa kuhusu ubora wa huduma tunazozipata, unajisikia uko salama zaidi unapojua vipimo vinafanywa kwa teknolojia ya kisasa na kwa usahihi mkubwa. Hii inaleta matumaini makubwa kwa sisi wagonjwa wa moyo”, alisisitiza Mzee Abdallah Said mkazi wa Pwani.
Naye Neema Joseph mkazi wa Dodoma alieleza kufurahishwa na mfumo wa kuweka miadi kwa njia ya mtandao huku akisema umepunguza muda wa kusubiri huduma hospitalini.
“Ninaweka miadi nikiwa nyumbani, nikifika hospitali napata huduma kwa wakati niliopanga. Hakuna tena kukaa foleni muda mrefu”, alisema Neema.
The Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) has inaugurated a modern laboratory equipped with artificial intelligence (AI) and robotic sample-processing systems, making it the largest of its kind in East Africa and Sub-Saharan Africa.
The new facility is designed to improve diagnostic accuracy, reduce human error, and enable early detection of diseases.
Speaking to journalists on Thursday, April 9, 2026, JKCI Chief Executive Officer Peter Kisenge said the investment is part of the Sixth Phase Government’s efforts, through the Ministry of Health, to ensure patients receive faster and higher-quality services.
“This laboratory has a modern system capable of analysing samples precisely, reducing human error, and detecting diseases even at their earliest stages,” he said.
The facility has cut waiting times for test results from three hours to just one and can process large volumes of samples quickly, helping reduce patient congestion.
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 11, 2026, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima na Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria. Hafla hiyo imefanyika kwa njia ya mtandao huku Rais akifuatilia akiwa Ikulu, Dodoma.
Chuo hicho kimempa heshima hiyo kutambua mchango wake mkubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuimarisha afya ya mama na mtoto, kuendeleza uongozi wa wanawake barani Afrika pamoja na kusimamia ajenda za biashara, hususan kwa vijana.
Kutunukiwa kwa heshima hii kuna manufaa makubwa kwa Tanzania kimataifa na kitaifa. Kwanza, kunaiweka Tanzania katika ramani ya nchi zinazoongoza katika ajenda za maendeleo endelevu, hasa katika sekta ya nishati safi na afya ya jamii. Pili, kunaimarisha diplomasia ya kimataifa kwa kuongeza ushawishi wa Tanzania katika Afrika na duniani, jambo linaloweza kuvutia uwekezaji na ushirikiano wa kimkakati.
Aidha, heshima hiyo inaongeza hadhi ya nchi katika kukuza usawa wa kijinsia na uongozi wa wanawake, ikiwa ni mfano chanya kwa mataifa mengine. Pia, inawapa motisha vijana wa Kitanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na ubunifu, wakitambua kuwa juhudi zao zinaweza kutambulika kimataifa.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kutunukiwa shahada za heshima. Awali, ametunukiwa shahada mbalimbali kutoka vyuo vikuu tofauti duniani.
Shahada ya kwanza ya heshima ya udaktari, alitunukiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 30, mwaka 2022.
Hiyo ilifuatiwa na shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India, Oktoba 10, 2023.
Tunu ya shahada hizo haikuishia hapo, mkuu huyo wa nchi alitunukiwa shahada nyinyine ya heshima ya udaktari ya Usimamizi wa Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Desemba 28, 2023.
Kama hiyo haitoshi Aprili 18, 2024, Rais Samia ametunukiwa shahada nyingine ya heshima na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.
Kwa ujumla, tuzo hizi zinaakisi namna ambavyo uongozi wa Rais Samia unavyotambulika kimataifa na kuthaminiwa kama mfano wa mageuzi chanya barani Afrika.
Kutunukiwa kwa Shahada hii ya Uzamivu ya Heshima ni uthibitisho wa nafasi ya Tanzania kama taifa linalochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ni heshima si kwa Rais pekee, bali kwa Watanzania wote, na inaendelea kuimarisha taswira ya nchi katika jukwaa la kimataifa.
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imesaini mkataba wa upangishaji ardhi na kampuni ya HWTZ SEZ Limited kwa ajili ya ujenzi wa kongani kubwa ya viwanda katika eneo la Bagamoyo Eco Maritime City.
Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri amesema mradi huo utatekelezwa katika eneo la hekta 500, sawa na asilimia 5 ya eneo la Bagamoyo SEZ, na ardhi hiyo imepangishwa kwa kipindi cha miaka 33.
Ameeleza kuwa uwekezaji huo utahusisha ujenzi wa miundombinu muhimu ikiwemo barabara, maji, umeme, pamoja na matumizi ya nishati jadidifu kama umeme wa jua. Pia, kabla ya mwisho wa mwaka 2026, viwanda vitatu vinatarajiwa kukamilika, ambavyo ni kiwanda cha kuunganisha magari, boti za uvuvi, kiwanda pikipiki, kiwanda cha vifaa vya ujenzi pamoja na kiwanda cha utengenezaji wa vipuri vya chuma.
Aidha, amesema mradi huo utagharimu takribani Dola za Kimarekani bilioni 3 (TZS trilioni 7.8) na unatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 5,000 za moja kwa moja kwa vijana pamoja na kuleta teknolojia za kisasa nchini. Kiwanda cha magari kitatumia nishati safi ya gesi asilia, hatua itakayochochea matumizi ya rasilimali za ndani na kupunguza uagizaji wa mafuta kutoka nje.
Amesisitiza kuwa ardhi ya uwekezaji haiuzwi bali hupangishwa kwa mujibu wa sheria, huku kukiwa na vipengele maalum vinavyolenga kuhakikisha wawekezaji wanatekeleza walicho ahidi kufanya. Pia ametoa rai kwa watanzania kuwa fursa hiyo si tu kwa wageni bali hata kwa wawekezaji wazawa wafike katika mamlaka ya TISEZA kuweza kupata vibali vya kuanzisha kongani za viwanda awe mtu binafsi au kwa kuungana na wengine watapewa kipaumbele.
Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kujenga uchumi shindani wa viwanda na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
